SIRI ZILIZOMO NDANI MAHUSIANO



Siri 6 Muhimu Zinazofanya Mahusiano Kudumu Katika Hali Ngumu

Labda nianze kwa kusema kuwa ndoa nyingi ama mahusiano mara nyingi yana migogoro na hii ni hali ngumu sana ambapo ndoa/mahusiano hupitia. Zipo ndoa ambazo hupata hali ngumu na kufikia kuachana kabisa eti kwasababu ya uchumi, Hapa pana njia kadhaa zitakazo epusha haya yasitokee.
 
1. TAMBUA NA FANYIA KAZI TATIZO.
Wakati joto la tatizo limepanda sio wakati wa kuwa na hasira juu ya mwenzi wako. Unapokuwa na matatizo, na hata kukusababisha shinikizo la damu kwako na saa fulani unakosa mwelekeo. Na hii inasababisha kutoelewana na mtu yeyote karibu yako, na pia unaanza kujitenga na kuwa peke yako, lakini yakupasa kugeuka na kumwambia mwenzi wako kuwa “ angalia tupo katika hali ngumu, na kuishugulikia hii hali wote kwa pamoja.
2. Tambua mambo yanayokufanya kuwa na misongo katika uhusiano wako.
Kwa uzoefu tu, hata taifa huwa linaporomoka kiuchumi pia, hivyo inakupasa  kumbuka kuwa tatizo si mwenzi wako, bali kutokuwepo na utunzaji mzuri wa mshaara, au kukosa kazi na hata pia uwepo wa madeni mengi. Hivyo yakupasa kuelekeza shabaha yako mahali pazuri. Kwasababu ukishagundua tatizo ni vyema kujaribu kushirkiana kwa pamoja katika kutatua tatizo kwa kutoa njia sahihi zitakazotumika kutatua tatizo.
3. Kuwa mkewli katika hisia zako.
Mawasiliano mazuri yenye uhakika chanzo chake ni ukweli na kuwa wazi. Kama umeaga kuwa unaenda kutafuta kazi sehemu fulani basi fanya ulichokipeleka. Usiseme kuwa unakwenda kutafuta kazi huku humanishi hivyo. Kuwa tu muwazi kwa kila kitu huku ukiruhusu mambo mengine kutoka kwa mwenzako.
4. Jisikie kuomba msaada pale unapohitaji msaada.
Hebu jihisi kuwa ndani ya shimo refu, na pia unajitahidi kusumuka jiwe kubwa kwenda kwenye mlima mwenyewe. Kama mkiwa wawili mnavuta wote mtafika kilimani wawili, kama mmoja wenu anasukuma kushoto na mwingine anasukuma kulia manapoteza nguvu nyingi huku jiwe halisogei. Usiwe mwoga katika kuomba msaada kwasababu kamwe huwezi kuongoza familia wewe mwenyewe.
5. Orodhesha vipaumbele na magoli yako
Hii si kwasababu ya hela zako ulizonazo, weka orodha ya hivyo vitu, thamani yake ya vitu ambavyo wote vitawapa heshima. Hii ni kama kampuni na hivyo  yahitaji kufanya kikao cha bodi na cha tathmini.
6.  Kuwa na mpango kazi.
Njozi huleta muamko na huamasisha kupata nyota njema katika maisha lakini muda fulani yakupasa kuweka kichwa chako katika mawingu. Tofauti kati ya njozi na mpango kazi ni muda haya mambo yanavyotendeka. Unatakiwa kujifanyia tathimini na kujigundua ulivyo, “ je ninasonga mbele? Tenga muda wako wewe na mwenzi wako mjitathimini na hivyo kupanga mipango kazi.