Upendo
ni hisia halisi za hiari toka ndani ya moyo wa mtu kwa mtu ampendaye mbali
napesa. Natambua kuwa unatambua jinsi ambavyo ni vigumu kuulinda upendo ili
udumu kuwa hai. Usipokuwa makini hatua zote za mwanzo na juhudi zote ulizotumia
kuupata zaweza kuwa ni bure, kama utakubali pesa iingilie upendo wako kwa
umpendaye. Waweza kujiuliza mwenyewe utafanya nini wakati pesa itakapo ingila
upendo wako?.
Wakati
matatizo yanapo ibuka kwa mara ya kwanza ni lazima ujiulize “kuna uhusiano gani
kati yangu na pesa?” pesa yaweza kuwa na maana tofauti tofauti kwa watu wengi
na hivyo hupelekea kwenye mada ngumu saana kuhusu pesa. Usipokuwa na pesa
kabisa ni lazima uwe na hofu kubwa saana. Ukiwa na pesa saana napo ni taabu, je
pesa humaanisha nini kwako?.
Pesa
haiwezi kabisa kununua upendo nafahamu hata wewe unalitambua hilo, pesa na
chombo cha biashara, unapo ingiza pesa kwenye upendo maana yake ni kwamba
unafanya upendo wako kuwa biashara. Ni kweli kwamba pesa ni muhimu katika
maisha yetu, huchukua nafasi kwenye mifuko yetu, hutusaidia tuwe na afya njema
lakini haina nafasi yoyote katika mioyo yetu.
Katika
kila mahusiano, kuna uwiano kati ya majukumu na nguvu ama uwezo. Mmoja wenu
anaweza kuwa ana nguvu saana kuliko mwingine katika kutoa maamuzi au mwingine
akawa ndiye mnyonge saana katika mahusiano yenu katika mahusiano yenu. Uwiano
sahihi katika mahusiano ni jambo muhimu saana ni kama tu mzani. Ikitokea
mwingine amemzidi mwingine katika uwiano wenu hapo shida huenda ikatokea.
Changamoto
za kiuchumi ni kitu kibaya saana katika mahusiano, madeni, uoga, ukaidi ni
miongoni mwa vitu vinavyo haribu saana uwiano huu katika mahusiano yenu na
hatimaye hali ya amani yaweza kutoweshwa. Hali ya kutoaminiana yaweza kuanza
kuibuka. Kukatishana tama kunaweza kufunika upendo wenu wa dhati. Hofu na uoga
ni sumu mbaya saana katika kuaminiana kwa wapenzi
Pesa
ni kitu ambacho husuluhusha matatizo yote ambayo mwanadamu aweza kuyapata nje
ya yale ambayo ni ya moyoni. Pesa ukiipata hata namna ya kufikiri hubadilika.
Lakini changamoto za kifedha hutowesha kabisa hata amani katka mahusiano, pesa
hufunika kabisa changamoto za ndani kabisa za mtu, hutowesha kabisa upweke na
aibu. Kukosekana kwa pesa hupelekea kila mtu katika mahusiano kupambana na hali
ngumu ya maisha na hivyo pesa huathiri hata mfumo na uwiano sahihi katika
mahusiano.
Katika
siku hizi mahangaiko ya kutafuta pesa na hali ya kutokuwa na kazi vina athiri
saana uwiano sahihi na upendo halisi kwa wapendanao. Hivyo zinahitajika juhudi
nyingi saana ili kurudisha nguvu inayoshikilia upendo wenu, la sivyo hali
yaweza kuwa mbaya katika mahusiano yenu.
Yatafakarini
maisha mnayoyaishi kwa mtazamo mpana saana. Pesa yaweza kuwafanya mtengane,
lakini ki msingi ni kitu cha kupita tu. Angalieni maisha yenu ya baadaye! Na
wala si ya leo na kesho tu. Kumbushaneni kwa pamoja malengo yenu na maamuzi
yenu mliyojiwekea.
Malengo
ya baadaye mliyojiwekea ndiyo yatawapa mwanga wa kupambana na changamoto ambazo
zinawapata kwa muda tu, malengo hayo yatawafanya mpate suluhisho la changamoto
mzipatazo. Songeni mbele huku mkiangalia malengo yenu.
Kwa
pamoja, ongeeni kwa upole na upendo kuhusu hofu inayowapata juu pesa mkitumia
uwezo mlionao kwa wakati huu. Furahini kwa kuwa pamoja katika wakati huu mnao
upitia, chekeni pamoja maana kicheko hubadili giza kuwa mwanga, mshike kwa
upendo mwenzi wako kila wakati wote kama ishara ya mapenzi ya dhati katika
kipindi kigumu mnachopitia.
Ifanye
ahadi ya upendo wako kwa mwenzi wako kuwa mpya kila wiki au kila siku. Kama
wewe umeolewa au umeoa ahadi yako uliyo itoa siku ya harusi yako endelea
kuifanya kuwa mpya. Kama bado unamtafuta na bado hamja oana, endelea kumuonesha
kuwa umpendaye kuwa yeye ni wathamani kuliko chochote kile.
Mara
nyingi saana pesa humomonyoa na huweka kutu katika chuma cha upendo, pesa ni
changamoto kubwa saana ya upendo wa dhati. Pia pesa ni nguvu ambayo yaweza
kuleta hali ya kutoelewana katika mahusiano kama hatutaweza kuitumia vizuri.
Wapenzi wapya au wale walio wachanga katika mahusiano ni
rahisi saana kupatwa na changamoto hii ya pesa katika mahusiano yao kuliko wale
waliyo na uzoefu au wale waliyo ishi pamoja kwa muda mrefu. Changamoto ni kitu
cha kawaida. Uchumba au kuchunguzana ni kama mtu ambaye anachagua bidhaa
dukani, kujaribu na kumchunguza mwenzi ambaye anafaa ni jambo la muhimu saana
kabla ya kuoa au kuolewa. Chunguza jinsi mchumba wako huyo anavyo tumia pesa,
itakusaidia saana kutambua jinsi ambavyo mchumba wako huyo atakavyo kuwa
baadaye, kuwa mwangalifu saana. Je anatumia pesa kwa uangalifu?. Je anaweka
akiba kwa ajili ya baadaye au ndiyo anazitumia na zinaisha?
Leo
ni kawaida kabisa kuwa na hofu juu ya Hali ya kiuchumi katika familia nyingi,
hili haliepukiki. Kila mmoja ana mzigo wa kufanya pesa nayo haitoshi, dunia
nayo haijiwezi kila siku tunashuhudia hali ya kutokuwa imara kiuchumi je hali
hii katika mahusiano yako unaichukuliaje?