Thursday, July 31, 2014

SIRI 6 ZA AJABU ZINAZOIMARISHA UHUSIANO.




Uajabu wa kitu ni vile kilivyo cha pekee na kinavyofanya kazi tofauti na vingine. Tangu nimegundua siri hizi mahusiano yangu na rafiki yangu wa kike yameimarika na kuwa na furaha siku ziongezekapo, nawe ukizitumia hakika yangu ni kwamba uhusiano utaimarika kwa namna ya ajabu. Ili kuwa na mahusiano yenye kufanikiwa ni lazima kujua unafanyaje ili uhusiano wenu uwe ni wa kudumu. Zifuatazo ndizo siri 6 muhimu za kuzingatia pale unapozigundua. 
1.     KUWA NA URAFIKI WA KUDUMU
Jiulize mwenyewe kuwa ni urafiki wa aina gani ulikuwa nao kwa rafiki yako, fikiria mambo ambayo yanakufanya kufarahi na marafiki wengine mbali na mwenzi wako kama vile utani ulio mzuri na mambo mengine. Pia ni vema kuyatumia hayo bila siri katika mahusiano yenu. Kama unataka rafiki mzuri pia unatakiwa kuwa rafiki mzuri.
2.     KUTANA NA MAHITAJI YA WATU.
Kwa uhusiano uliofanikiwa ni mahala pazuri ambapo mahitaji ya watu wawili hukutanishwa. Jaribu kujihoji nini ambacho mwenzi wako anahitaji ili kuwa tayari kumtimizia hitaji lake. Huenda kwa namna moja anataka sehemu laini ya kuangukia ama anahitaji bega zuri kwaajili ya kuwa mahali pake pa kulilia. Na hii haiitaji kujadiliana na kujua mahitaji ya mwenzi ama mchumba lakini tu jitahidi kugundua bila yeye kujua kuwa ni yapi mahitaji yake na umtimizie hata kama ni anapenda kuambiwa kuwa umependeza wewe fanya hivyo.
3.     JIWEKEE MALENGO.
“Amka kila siku asubuhi na kujiuliza, nini nitakachokifanya leo kipya? Hata ijapokuwa ni mambo madogo lakini yakiunganishwa kila siku yanaleta tofauti katika mahusiano. Tafuta sehemu iliyotulia kila siku na kufikiria kwa makini juu ya jambo gani jipya utalifanya na pia kuweka  malengo ya mahusiano yenu, unaweza  kumpigia mchumba wako masaa ya mchana kumsalimu na kumjulia hali, au kumwambia tu kuwa unampenda sana. Jitahidi sana kwa hili.
4. ZINGATIA MAMBO YA MSINGI.
Hapa jambo la msingi ni kuelewa kuwa jambo mnalolilenga ambalo ni ndoa linapaswa kuwaje, pia linataka mambo gani na ili lifanikiwe, linahitaji kuwa na vitu gani na hivyo kuanza kuyafanya hivyo vinavyohitajika. Tafakari kwa undani juu ya mafanikio ya mauhusiano yenu  na kuishi kuligana na misingi hiyo itakayowapelekea katika mahusiano wenye  mafanikio. Ishi kulingana na matazamio yatakayowaletea tofauti katika maisha  yenu.
5.CHUKUA HATUA.
Kamwe huwezi kumuongoza rafiki yako nmna anavyoweza kuishi kwenye uhusiano, lakini unaweza kuzuia mazingira hasi katika uhusiano. Unatakiwa kuchukua asilimia mia moja ya wajibu wako kwa namna unavyoenenda katika uhusiano. Pia amua kile unachokiamini na kukifanya kuwa cha kweli na kukifanya kuwa sahihi asilimia mia.
6. BADILI MITAZAMO HASI KUWA KATIKA ORODHA YA MAJUKUMU.
Baada ya kuanguka katika nyanja fulani fulani za mahusiano badili mitazamo na majibu yote hasi na kuwa katika mitazamo chanya. Kwa mfano kama hauna furaha na yule umpendaye inakupasa kutafuta na kuandaa orodha ya vitu utakamvyomfanyia mwenzi wako awe na furaha kwa hakika mkiwa pamoja nae.