Siri
ya kudumisha ndoa yenye furaha ni pamoja na kumuoa au kuolewa na mtu ambaye ni
rafiki yako. Kwa maana nyingine urafiki mwema hupelekea kuwa na ndoa yenye
furaha baadaye. Mnaweza kuishi kama marafiki mkicheza na kufurahi
kuwa pamoja muda wote. Msitegemee kuwa tendo la ndoa pekee ndilo lijenge ndoa
yenu hapo mtakuwa mnajidanganya, fikiria kama ikitokea kwa bahati mbaya mmoja
wenu akafanyiwa upasuaji utakao pelekea kutofanya tendo la ndoa je mtaendelea kuifurahia
ndoa yenu au ndio mtaishia hapo?. Hakikisha hukati mawasiliano na mke au mume
wako, likitokea jambo linalowakwaza, kaeni ninyi wawili mlimalize. Hakikisheni
mnadumisha upendo wenu wa kwanza mlio anza nao. Kumbuka ndoa ni kitu kigumu
kinahitaji kila mmoja kujitoa kikamilifu kwa mwenzake pamoja na kumuona
mwenzake ni wamuhimu saana kwake. Hapa tutaangalia mambo mbalimbali
yatakayopelekea wewe udumu kuwa a ndoa yenye furaha.
Siri
za kuwa na ndoa yenye furaha.Ndoa ambayo itadumu kuwa na furaha katika muda
wote wa maisha yao ni ile ambayo wanandoa wataelewana, wanasoma vitabu pamoja,
wanahudhuria semina mbalimbali pamoja, watasoma machapisho mbalimbali yahusuyo
ndoa kwenye mtandao pamoja na kuona mfano wa ndoa zingine ambazo zina mahusiano
mema na kujifunza kwazo pamoja.
Yafuatayo
ni mambo ambayo kama yakifuatwa na wanandoa kikamilifu yaweza kuwafanya
wanandoa kuishi kwa furaha katika maisha yao ya ndoa.
1. Usikate mawasiliano.
Kumbuka
siku unakutana na mchumba wako kwa mara ya kwanza mlielewana kwa njia ya
mawasiliano , hivyo bila mawasiliano mazuri na mke au mume wako fahamu kwamba
ndoa yenu iko kwenye matatizo. Kuongea pamoja, kuelezana pamoja kile
ambacho kila mmoja anakihitaji katika maisha yenu ya ndoa huleta maelewano mema
kati yenu. Ni kweli kwamba kadri ambavyo mnavyozidi kuishi pamoja mawasiliano
yaweza kupungua kwa sababu ya kuzoeana saana lakini kamwe msiruhusu kabisa
mawasiliano kukatika. Mawasiliano mema kati yenu ni muhimu katika kuelewa
hitaji la mwenzako na huleta furaha katika mahusiano yenu. Mawasiliano ni
muhimu, tumia maneno mengi zaidi kuwasiliana na Yule uliyemchagua kuishi naye
japo vitendo ni muhimu zaidi kama kumshika mkono, kumkumbatia, kumvalisha,
kuvaa nguo wewe mwenyewe nguo nzuri, jipulizie pafumu ile ambayo mchumba wako
anaipenda, mpe zawadi japo ni ndogo na za kawaida, vitu hivi huboresha saana
mawasiliano ya wana ndoa.
2. Sikilizaneni.
Masikilizano
mema ni muhimu kwa afya ya ndoa yenu. Kuwa tayari muda wote kumsikiliza
mwenzako. Baada ya ratiba ngumu za siku kuwa na hamu ya kumsikiliza mwenzako
kwa kumuuliza maswali mbalimbali, lakini kumbuka- wakati mwingine hata mke au
mume wako naye anahitaji kuku uliza au kukusikiliza, hivyo epuka saana kutoa
hitimisho wewe tu!, fungua masikio yako na msikilize kile anachosema mwenzako.
3. Ucheshi na ukweli.
Moja
ya kitu muhimu saana katika kuwa na familia au ndoa bora ni ucheshi kwa wana
ndoa. Ni vigumu saana kubaki na hali ya kufahi na kucheka pamoja lakini mnaweza
kufanikiwa katika hili kwa kutembelea wote katika maeneo mapya kwa pamoja mkiwa
wenyewe tu wewe na mume ama mke wako.
Kuwa
muwazi na mkweni ni msingi muhimu saana kwa wanandoa, hakikisha unakuwa mkweli
kwa mke au mume wako hiyo itawafanya muaminiane wote na ndoa yenu itakuwa
ni ya furaha siku zote.
4. Onesha upendo.
Hakikisha
unatumia muda mwingi kuongea na Yule umpendaye. Unaweza kuwa mbali na mume au
mke wako lakini unaweza kumudu kuongea na umpendaye hata kwa njia ya simu, ili
mradi tu onesha kuwa unampenda na kumjali.
Onesha
unampenda saana mke au mume wako daima. Kila siku hakikisha unadhihirisha
upendo wako kwake usichoke. Mbusu mke au mume wako, mkumbatie kila mara kama
ishara ya upendo. Kama mtapendana kwa dhati basi bila shaka mtaheshimiana, na
kila mmoja atamthamini mwenzake. kila siku tafakari kwa nini ulimpenda yeye tu
na wala si mwingine, hii itakufanya umpende zaidi mke au mume wako.
5. Mthamini mke au mume wako.
Ili
kila mmoja awe na amani katika ndoa ni lazima kila mmoja awe na mchango sawa
katika mahusiano. Usioneshe kuwa wewe ni bora kuliko mwenzi wako hii ita
mfanya mwenzako ajisikie hana uhuru. Hii ita hafifisha mahusiano yenu kama mke
au mume.
6. Furahi pamoja na mke au mume wako.
Kudumisha
upendo kwa wanandoa ni rahisi tu, furahia kuwa pamoja na umpendaye, ongeeni
pamoja, fanyeni mambo mbalimbali ya kifamilia pamoja na kwa upendo.Wakati watu
wawili wanapoishi pamoja, ni lazima tu watu hawa watatofautiana kwa baadhi ya
mambo kwa sababu binadamu wote tunatofautiana namna tunavyo fikiri na kutoa
maamuzi. Wakati hali hii ya kutoelewana inapotokea kwa wana ndoa, tumieni
hekima saana kumaliza tofauti hizo, ili kuacha upendo wenu uzidi kuwa imara na
wala si dhaifu.
7. Samehe na kusahau.
Wana
ndoa wanaofanikiwa katika maisha yao ya ndoa ni wale wanao pokea na kutoa
msamaha. Ni wale wanao samehe na kusahau kabisa makosa ya wapenzi wao. Wakati
wanapofanya makosa ambayo yanawaumiza wapenzi wao wao wana omba msamaha. Hivyo
kusameheana ni jambo la muhimu saana katika mahusiano.
8. Kuvumiliana.
Wanandoa
wanaofanikiwa kuishi muda mrefu wakiwa nafuraha daima ni walewanaovumilia hali
zote za maisha. Mfano wakati wa magonjwa, wakati wa utajiri, wakati wa
umaskini, wakati wa afya njema. Kama wanandoa wataweza kuvumiliana katika
hali zote hizi basi wataishi kwa furah kwa sababu watakuwa wamezipitia nyakati
zote hizi, hivyo kila mmoja atamuona mwenzake ni muhimu zaidi.
9. Muwazie mema mke au mume wako.
Ndoa
nyingi zimekuwa zikifurahia maisha ya ndoa kwa sababu wote wanawaziana mema.
Mhurumie umpendaye, mjali mtie nguvu pale ambapo anakata tama, weka upendo wako
wote kwake.