Je
mpenzi wako anahitaji kuwa na wewe muda wote? Tangu nigundue siri hii
nimependwa mara mbili zaidi nilivyopendwa wakati wa uchumba. Naamini baada ya
kugundua na wewe kama mimi hautaamini jinsi unavyopendwa… Watu huwa
na tabia yakuonyesha upendo wa juu sana kwa jinsi ya tofauti na wengine
huonekana kama kutokufahamu nini humaanisha. Ingawa kila mtu hutakiwa kujua
namna ya kuuyeyusha moyo wa mwenzi wake kwasababu ni hatua ya mwisho ya
kumshawishi mwenzi wako.
Kwaaajili ya mke wako/rafiki yako wa
kike.
1. Umshtushe mke wako siku moja na
mandari (mtoko). Panga mahali pa kukutania siku za wikiendi au siku yoyote
ambapo mna siku ya mapumziko. Hakikisha kuwa hana ratiba yoyote nyingine zaidi
ya hiyo. Ndipo unapomwambia kuwa aambatane na wewe mwende kwenye supermarket au
kitu kifananacho na hiki. Mpe muda wa kujiandaa vizuri, muda wa kuingia kwenye
gari, na munaweza kubeba hata vyakula laini ama vipoza njaa. Mpeleke mwenzi
wako kwenye bustani nzuuri maarufu kama beach na mwambie kuwa unampenda na
ndiyo maana umeeandaa hili tukio ili kumdhihirishia ni jinsi gani unampenda.
2.
Mwandikie mashairi. Na kama hii sio hobi yako pia zipo sehemu nyingi zenye
mvuto. Jaribu kumsomea kitabu cha mashahiri yenye ujumbe wa kumsifia, nyimbo za
upendo n.k. usirudie neno lolote kwasababu itazoeleka na atakudharau.
3.
Mpikie chakula kizuri na kitamu, washa mishumaa punguza mwanga wa taa na
safisha nyumba. Na atakapofika nyumbani atakosa cha kusema.
4.
Shika mkono wake kila mara mnapokwenda mahali popote nje na nyumbani. Kama hili
haliwezekani {kwasababu mmoja wenu amebeba mototo} hakikisha unaendeleza
mawasiliano ya nje. Hii itamfanya ajisikie kuwa unajivunia ukiwa nae na kamwe
huwezi kumuacha.
5.
Panga ratiba ya kupiga picha. Mpe nafasi mke wako ama rafiki wako wa kike
ajipambe kwaajili yako, pia chukua picha zake ambazo utaweka kwenye pochi yako,
ofisini ama kwenye gari lako. Mwambie kwamba yeye ni mzuri na kuwa amepiga picha
nzuri.
6.
Pata muda mchache wa kwake siku moja na umwandikie neno rahisi tu
“Nakupenda” na bandika popote pale. Bandika hilo neno bafuni kwenye kioo
ama sehemu ambao kwa haikka ataona huo ujumbe. Hii huimarisha na kumfanya yeye
kuwa wa pekee sana kwako na kukupenda sana. Na kama unahitaji kupanua wazo hili
unaweza kumuachia ujumbe mtamu katika maeneo yake machache pale unapotoka.
7.
Kama wewe ni mchoraji unaweza ukapata hamasa na kuchora Titanic, ukapaka rangi
ama kumchora umpendaye. Utapata majibu mazuri kama amani yako imeimarishwa na
kama bado mwambie kwamba huwezi kuumba kitu kizuri sana kama wewe.
Kwa mume wako/rafiki yako wa kiume.
1. Baada ya kazi ngumu za wiki,
mwandikie ujumbe mzuri sana wa kurudi nyumbani. Mtumie ujumbe wa upendo wa kumsihi
aje nyumbani na pia wa kumkumbusha kuwa ni muda mwafaka wa kupumzika na wewe.
2.
Vaa nguo za chumbani huku ukimsubiri atoke kazini. Hii itamfanya kukupenda
zaidi. Na kwa hakika atakubali jitahada zako na itamuongezea upendo kwako.
3.
Kama mwezi wako anarekebisha uso wake kama kunyoa ndevu, mfanyie hilo. Weka
nyimbo za upendo kwa taratibu na kwa upole mnyoe. Wewe chukua muda wako na
fanya hivi atajisikia kuwa anapendwa na anajaliwa.
4.
Chukua muda wako mkiangaliana machoni. Kubali na tambua uwepo wake, tambua
marashi na manukato yake na joto lake. Na kama unajisikia hata kumbusu fanya
hivo.
5.
Jifanye kumuhitaji. Mwanaume hutamani kuonekana kuwa yeye pekee ndiye
anayekulinda, hivyo mwambie kuwa hujisikii vizuri na huwa unakuwa mpweke pale
anapokosekana ama unajisikia vizuri na kuwa na amani pale anapokuwepo.
6.
Mkumbatie kwa ghafla. Onyo-fanya hivi pale ambapo mpo wawili tu ili kwamba
asije akajisikia kuwa hayuko huru au amelazimishwa. Napendekeza fanya hivyo kwa
muda wa dakika 5-6 afu mpe nafasi.
7.Mnunulie
tiketi ya mpira wa miguu au mpira wa kikapu ule ambao yeye angependa kuuona.
Ili kuonyesha upendo nenda nae mkashabikie timu yake kwa pamoja.