Thursday, July 31, 2014

SIRI AJABU ILIYOMO NDANI YA MAHUSIANO



Watu wengi wanapata uzoefu wa mapenzi kutoka kwenye maadili ya tamaduni mbalimbali zinazofahamika. Tunaamini kuwa mapenzi yanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha. Mtazamo wa kimapenzi unaotokana na tamaduni mbalimbali unajenga taswira ambazo sio sahihi, mitazamo yao ipo kwa ajili ya kuburudisha tu na wengi tunafikiria kuwa hayo ndiyo mapenzi. Mtu anapopenda mno kiasi cha kuwa na wazimu wa kimapenzi wengi huwa tunafikiria kuwa huo ndio upendo. Tatizo linalojitokeza ni kwamba tunapogusa dhana ya mapenzi ya dhati wengi wanakufa mioyo kwasababu kuna vitu vingi havipo kwenye maadili ya tamaduni zetu. Baadhi wanahitaji waone jinsi ya kupenda kulingana na maadili ya mapezi ya kweli. Inawezekana kabisa na sio kuwezekana tu lakini pia tunataka ubadilishe mtazamo wako wa kupenda. Hebu fuata mtiririko huu ili kupata kile unachokihitaji;- jinsi ya kupenda na kupendwa. • Tambua tofauti iliyopo kati ya tamaa na upendo. Tamaa ni hali ya kisaikolojia ambapo mtu anakuwa na upendo wa msisimko unaosababisha kuzalishwa kwa homoni za mwili, tamaa haidumu. • Mapenzi ni mbinu ya kujifunza, sio kitu kinachotokana na homoni au mhemko mtu mmoja alisema kuwa upendo ni”tendo la hiari” usipo jifunza jinsi ya kupenda ni dhahiri utaumizwa tu, hii ni kwasababu utakuwa huna uzoefu. • Jifunze mbinu za mawasiliano. Hii ndio njia pekee ya kukuza uamifu na ukaribu. Jinsi unavyozidi kuwasiliana na yule umpendae ndivyo unavyopunguza kiwango cha kuumizwa. Siku zote tofauti baina ya watu wawili huwa ipo, lakini kama mahusiano yanaenda sawasawa hizo tofauti zinamezwa, kitu muhimu ni kuzitambua tofauti zenu ili zisije zikavunja mahusiano yenu. Lazma utambue kuwa mwenzako anatoka wapi, yeye ni nani na pia uwe na uwezo wakujitambulisha kwake, zitambue tofauti zenu kwanza na kuzishughulikia ili kujenga mazingira yatakayokuwa salama kwa wote. • Usiweke mawazo yako kwenye vitu unavyopewa na mpenzi wako, na jinsi anavyokujali, angalia kuwa mpenzi wako nae anataka nini, unaweza kufanikisha hili endapo utajifunza jinsi ya kujali wengine. • Msaidie mtu mwingine. Mfadhaiko unamsababisha watu kujishughulisha na mambo yao binafsi hivyo hawajifunzi namna ya kupenda hivyo huumia pindi wanapoyaanza mapenzi. Unavyozidi kujali wengine ndivyo utakavyo jali mahusiano yako na mpenzi wako. • Uwe na uwezo wa kukusanya mawazo ya wegine ambao wako katika mahusiano, ukweli wanaokuambia kuhusu mapenzi yao unaweza ukawa ndio ukweli kuhusu mapenzi yenu pia, watu wenye mifadhaiko huwa wanaamini kuwa hakuna ukweli tofauti na mifadhaiko yao. • Weka wazi yaliyo moyoni mwako ambayo hujaridhishwa nayo. Kuhisi kukataliwa ndio mwanzo wa mfadhaiko. Tambua kuwa sauti iliyo moyoni mwako ina nguvu lakini sio sahihi, inakubidi useme kuwa mimi sijakataliwa na kama unaona kuna udhafu wowote jaribu kuuweka wazi kuliko kuweka dhana ya kukataliwa.