Kukatisha Mawasiliano.
Kama
mke amekudanganya wewe mme, lakini hupenda kuendelea kuishi katika ndoa, kwa
kawaida amekosa na amekuondolea heshima. Mbali na kumshushia heshima mumewe
lakini hutakiwa kusitisha mawasiliano kwa yule ambaye walishiriki kumdanganya
na kuepuka maeneo yote ambayo yatampelekea kukutana au kumkimbilia huyo mtu.
Hii ni kwasababu mwanamke anatakiwa kujisikia kuwa tatizo la udanganyifu
limekwisha na hata hisia zinazopelekea kukumbuka yaliyopita.
.Imarisha
mawasiliano.
Ingawa
inaweza kuumiza na kuumiza kujadili udanganyifu au ukosefu wa uaminifu
uliotendeka, ndoa inatakiwa kujengewa msingi wa ukweli na uwazi. Kuimarisha
mawasiliano juu ya jambo lilitokea ambalo likapelekea udanganyifu, na inaweza
kuwa ngumu sana kulijadili hili jambo kwa undani, lakini kwasababu ya kuweka
amani ya moyo ni vizuri. Kama mke anaendelea kutunza siri hii italeta tatizo
kubwa badala yake anatakiwa kuomba radhi na kuthamini hisia za mume wake
ili kuweka ndoa yake katika hali nzuri.
Anzisha mahusiano upya.
Baada
ya udanganyifu, ni vigumu sana kurudisha uhusiano kama ulivyokuwa mwanzo.
Katika kurudisha uamuzi wenu dhabiti, muanze uhusiano upya. Mwanamke anaweza
kumshtukiza mume wake na vitu vipya vitakavyoimarisha kama kumjali, upendo
ulioboreshwa yaani zaidi ya mwazo, hata kumkubatia kumbatia wakati wakiwa wote.
Pale mwanamke anapomdanganya mwanaume, mwanaume hujisikia kuwa kutotakiwa
katika jamii aliyopo na pia kutokuwa na mvuto. Kuwa nae karibu na kuonyesha
jinsi uliyoathirika katika jambo hilo kunamuinua na kumuongezea ujasiri na
kujiamini pia.
Tafuta washauri wa ndoa.
Kufanya
kazi na hisia za ndani za mtu aliyedanganywa na mke inahitaji mtu aliyebobea
katika ushauri kuhusu maswala ya mahusiano. Mshauri wa ndoa au wa familia yeye
atawasaidia wote katika kutatua migogoro na kutokuelewana kwenu, na pia hata
tabia mbaya za uvunjifu wa ndoa yenu na kuwapa njia bora zitakazofanya uhusiano
wenu au ndoa yenu kuuendelea, na itawasaidia kuwa na mtu wa tatu ambaye
atawasikiliza na kuwapa majibu yatakayoisaidia ndoa yako.