Thursday, July 31, 2014

JE UNAFAHAMU SIRI INAYOPELEKEA UPENDO WA KWELI?.




Yapo maswali mengi ambayo waweza kujiuliza wewe ambaye bado hujapata mtu akupendaye kwa dhati. Mojawapo ya maswali hayo ni Lini nitampata mtu ambaye nahitaji awe mwenzi wangu wa maisha? Na nitampataje Yule ninaye mhitaji? Karibu kila siku maswali kama haya huulizwa na vijana wengi ambao hawajapata wenzi wao. Waweza kujiuliza upendo ni nini? Kila mtu aweza kueleza jinsi ambavyo anaufahamu upendo, lakini nionavyo mimi upendo ni hisia ambayo mtu anaipata baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na mtu sahihi anaye muhitaji. Upendo ni zawadi ambayo MUNGU mwenyewe ametupa zawadi hiyo sisi wanadamu kati ya jinsia ya kike na ya kiume. Wapo watu baadhi wanao onesha kupenda bila kuwa na nyenzo sahihi zinazoweza kuwasaidia kutambua kuwa ni upendo wa kweli au ni wa ulaghai, namna ya kuupata, kuuendeleza na kuukuza ni sawa tu na kujaribu kuvua samaki baharini au ziwani bila kuwa na ndoano! Ni kitu ambacho kinasikitisha na kushangaza.
Waweza kujiuliza ni nyenzo zipi ambazo zaweza kukusaidia kuukamata upendo?. Zifuatazo ni siri 5 muhimu  ambazo zitakusaidia kuupata upendo wa dhati. Kama utaamua kuzitumia zitakufanya upate upendo wa dhati maana kwangu mimi zimeleta mabadiliko makubwa saana!
1. Jiheshimu.
Kama hujiamini wewe mwenyewe au kujiongoza mwili wako na maisha yako kwa nidhamu na heshima, mtu mwingine atakuheshimje na atakuaminije fahamu wazi kwamba hakuna mtu ambaye ataweza kufanya hivyo kwa ajili yako hivyo kama hutajiheshimu hata watu wengine hawata kuheshimu vilevile. Watu wengi wanapokuwa wanatafuta wenzi wao wa maisha hupenda saana kufahamu huyu mtu ninayetaka awe mwenzi wangu mwonekano wake ukoje? anamvuto? Pia maisha yake anayaendeshaje?, vitu gani anavyovipa kipaumbele katika maisha yake, ujuzi alio nao, malengo yake katika maisha yake. Haya ni mambo ambayo huzingatiwa saana katika kumpata umpendaye.
2. Mwonekano na utu.
Haihitaji mwanamke au mwanamume awe mtu mashuhuri, mwembamba au mrembo saana!. Zipo aina nyingi za uzuri kwa wanaume na wanawake ambazo ni muhimu kuzingatiwa wakati wa kuutafuta upendo mfano usafi, unadhifu namna ambavyo anaweza kuvaa vizuri vyote hivi kwa pamoja vinaunda mwonekano wa mtu. Pia watu wengi hupenda watu ambao wanaweza kusikiliza wenzi wao, kufurahi na kutabasamu hivi navyo huunda utu wa mtu. Hivyo kwa mtu ambaye anatafuta upendo wa dhati haikikisha mwonekano wako uwe na mvuto pia uwe na utu wema kwanza wewe!.
3. Usikate mawasiliano.
Mawasiliano ni kitu cha kawaida lakini ni kitu cha muhimu saana katika mahusiano. Hakikisha unakuwa na mawasiliano mazuri na Yule ambaye unadhani atakuwa mwenzi wako. Kama yuko mbali na wewe tumia mawasiliano ya simu.
4. Tafuta mwenzi ambaye yuko huru.
Ili kuondokana na maumivu ambayo unaweza kuyapata baadaye katika mahusiano, ni vyema kutafuta mwenzi ambaye hajawahi kuwa kwenye mahusiano hapo kabla. Takwimu nyingi huonesha kuwa watu wengi ambao walianza mahusiano mwanzo wakaja kuachana kuna uwezekano mkubwa wa kupendana tena baadaye hata kama mmoja wao au wote wakiwa na familia zao.
5. Hakikisha unampata anaye kupenda.
Hatimaye baada ya kuwa umempata unaye vutiwa naye na unayempenda kwa dhati kumbuka kumchukua au kuchukuliwa na Yule umpendaye. Kama utakuwa umempenda ambaye yeye hakupendi achana naye!. Maana ukimpata ambaye mnapendana yeye atajitahidi kukupenda na kuanza naye safari ya mahusiano kwa nia moja.