Moja
ya HUZUNI kuu maishani ni pale mwanaume au mwanamke anapoingia katika ndoa na
matumaini makubwa pamoja na matarajio makubwa sana, pale tu matarajio hayo na
matumaini hayo yanapoharibika baada ya miezi au miaka michache. Na hii hutokana
tu majuto mazito ayapatayo mwanandoa kutokana na kazi kubwa ambayo huyu
mwanaume mtanashati au mwanamke mzuri aliifanya awali nayo ni katika kummchagua
mwenzi wake wa maisha ambaye alidhania kuwa ni dhahabu kumbe ni chuma cha kutu
tena kilichoharibika. Huu uharibifu unapotokea haubakii tu kwa wazazi bali
huathiri hata kizazi kijacho. Je umewahi kujiuliza kuwa kwanini
haya yanatokea? Kitabu hiki kimebaini sababu zinazopelekea haya kutokea
na kutoa njia za kuelekea mafanikio ya mahusiano yaliyo na furaha hasa
tukijikita katika njia sahii na madhubuti za kutafuta mchumba.
NJIA SAHIHI ZA KUTAFUTA MCHUMBA
Uchumba
ni mahusiano mazuri yanayoendeshwa baina ya vijana wawili wa jinsia tofauti
yaani mwanamke na mwanaume kwa malengo ya kuwa na familia kati ya kijana wa
kiume na kijana wa kike. Na sababu ya mahusiano mazuri ya uchumba ni
kuingia katika ushirikiano makini kwa njia ya ndoa, kwa kuongezea mahusiano
haya ya uchumba yanalenga hasa katika kuwa na mtu ambaye anafaa na mtu muhimu
katika mahusiano ya ndoa. Pia washauri mbambali wanahusia kuwa
mahusiano haya ya uchumba yanawaruhusu hawa wapendanao kumjua mwenzake
kinagaubaga bila kuwa na mgandamizo wa kingono, mihemko au hisia za mwili.
Kumtafuta mchumba ama mwenzi anaekufaa mwenye tabia kama zako si uchaguzi
unaohusisha kumchagua mtu ambaye atakusaidia kuishi katika kipindi cha upweke.
Hii humanisha kuwa mwenzi ama mchumba utakae mchagua anapaswa kuwa ni yule
ambae katika ukuaji wenu miaka thelathini, hamsini na sitini ya uzeeni
bado utaendelea kumpenda. Kumchagua mwenzi ama mchumba wa maisha umakini wa hali
ya juu wa kijana awe yeyote unatakiwa mno, kujikabidhi
kikwelikweli katika biashara ya muhimu, na inahitaji wingi wa fikra makini,
utambuzi wa majukumu, zikiambatana na uwazi. Jambo la kuzingatia wewe kijana
ambaye unamsaka mtu muhimu katika maisha yako (mwenzi wako) ni kuwa usiingie
kwenye hii hatua ya uchumba mpaka jambo hili limedhihirika. Najua kwa
namna moja ama nyingine unaweza usinielewe ninalolimanisha, sasa basi haya ndio
mambo yatayokupelekea mpaka kufikia uamuzi wa kuingia katika mahusiano ya
uchumba na hata kuamua kutafuta mchumba unaye mtaka. Jambo mojawapo la kuelewa
hapa ni kwamba elewa kwa kina umuhimu wa maamuzi mazito unayo enda
kuyafanya kwa kuzingatia swala lenyewe la ndoa, na kifungo ambacho unaenda
kukianzisha kupitia mahusiano ya uchumba mda mchache kabla ya kuamua kuingia
katika uchumba. Ungana nami kupitia kitabu hiki kujifunza njia madhubuti za
kusaka umpendae mahali popote pale pale unapokua umefikia uamuzi huu makini wa
kumsaka yule unaemtaka kumkabidhi moyo wako kwa njia ya upendo wa kweli.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOCHAGUA MCHUMBA.
Hapa
chini nimekunyambulia mambo muhimu sana yakuzingatia wakati unataka kumchagua
yule unyemdhania kuwa ni mchumba wako kama ifuatayo,
1. AINISHA SIFA
UNAZOHITAJI KUTOKA KWA MTU UNAYEMTAKA.
Ingawa
inaweza kuwa vigumu sana kumjua aliye kamili na bora kwako hata ufunge macho na
wakati mwingine maneno kukuisha, hivyo basi unaweza kufikiria sifa unazozitaka
sana kutoka kwa mtu unayemtarajia awe nazo. Sifa ni za muhimu sana kwako kwasababu
zinakusaidia kumpata yule unaye mtaka, na hapa kuna mambo ya kufikiria
unapoainisha sifa wa yule anayekufaa:
a. DINI. Kama
wewe ni muyahudi kwa hakika utahitaji kuoa mtu aliye sawa na dini yako,
japokuwa unaweza kumbadilisha lakini marachache watu wamefanikiwa kwa hili ila
uwezekano wa kurudi katika dini ya awali kwa yule aliyebadilishwa ni
mkubwa.
b. MAADILI
YA KIFAMILIA.
Je
umedhamiria kuwa na watoto ama? Na kama ndivyo je ni watoto
wangapi? Ama si nia yenu kuwa na watoto katika hali yoyote? Ingawa
mnawezakubadili mawazo yenu lakini pia hili ni jambo la kuangalia wakati
unamtafuta mchumba wa kuoa ambaye mtashauriana na kushirikiana mawazo
(Ingawa hutakiwi kuliongelea hili mara tu unapokutana nae).
c.
UTU WAKO.
Ingawa
si rahisi kutabiri utu wa mtu lakini kuna mambo machache ambayo ni muhimu
kuyaangalia. Je mtu utakaemchagua ua furaha na uchangamfu wako au
anayeshirirki pendo lako kama kichekesho tu? Weka hili akilini unapomtafuta
mchumba anaekufaa.
d.
MTAZAMO KUHUSU UHUSIANO.
Je
mtu utakae kuwa naye je ni mtu ambaye ni tegemezi kimawazo? Ama ni mtu ambaye
anaweza kusimama peke yake kimawazo? Pale anapokuwa yeye kama yeye? Hili ni
jambo la msingi sana kulizingatia.
e.UHUSIANO
NA JAMII.
Je
mtu unayetaka kuwa naye ni mcheshi? Je anashirikiana na jamii inayomzunguka?
Vipi kuhusu jamii anayoishi nayo inamtafsiri kama msaada kwa jamii ama kero kwa
jamii. Je marafiki alionao ni wa aina gani? Upo msemo unosema kuwa
nionyeshe marafiki zako nikwambie tabia yako Je anapenda kuwa na marafiki wa
matawi ya juu tu au wa aina zote? Hili pia ni muhimu sana kulizingatia.
f.
NIA ZENU.
Mara
nyingine mtu uliyempenda mnaweza msiwe na nia moja kwa pamoja, au kuwa na
matakwa ya pamoja, unatakiwa kuwa na mambo machache ambayo yanaendana kwa
pamoja na yule umpendaye ambayo wote mnapendezwa nayo kwa pamoja ambayo
yatafanya mahusiano yenu kuendelea vizuri. Kama wewe tabia yako ni kupenda
kusoma vitabu na umpendaye hapendi hiyo tabia utakosa vitu vya kuzungumza
nae.
2. USIRIDHIKE
Watu
wengi sana wameridhika sana kwasababu wamewapata watu amabao wanawafanya
wao kutokujisikia upweke na kuwa wamependwa hata kama si kwa njia iliyo sahihi.
Sababu nyingine ambayo inawafanya watu waridhike ni kwamba wamekuwa na
mahusiano labda kwa miaka mitano na kugundua kuwa wanaweza siku moja wakawa ni
mke na mume hivo basi kwasababu hii ya kukaa muda mrefu katika mahusiano wengi
wameichukua hatua mojawapo. Lakini msisitizo ni huu kuwa tafuta mtu ambaye
unamtaka lakini si kwasababu watu wanataka umuoe au kwasababu wanampenda, ama
kwasababu familia inataka uwe nae, au kwasababu unaona aibu kusema kwaheri kwa
rafiki wa awali uliyekuwa nae na kujiuliza maswali atanifikiriaje mimi hali
ukizingatia tumekuwa nae katika urafiki kwa muda mrefu! Lakini ipo kauli moja
kuwa tafuta mtu unayempenda.
3. KUWA
TAYARI KUKUBALIANA NA BAADHI YA MAMBO
Ijapokuwa
umetengeneza orodha ya vitu uvipendavyo na vile usivyovipenda haijalishi ni
sehemu gani, itakusaidia sana ambavyo vitakufanya uwe nafuraha, ukweli ni
kwamba hautapata mtu ambaye ni mkamilifu asilimia mia, lakini mtu sahihi kwako
ni yule anaekufanya kuwa ni mwenyefuraha muda mwingi, na mtu huyo anakidhi pia
mahitaji ambayo kwa namna fulani hukujua kama unayo. Usikatae kumchagua mtu
eti kwasababu hakidhi vigezo vyako vyote hasa katika kukidhi mahitaji
yako yote, kwasababu hayupo. Lakini usikae na mtu ambaye unadhania kuwa
hakidhi vigezo ama sifa za msingi kwako, ingawa unapaswa kuwa ni mtu usiye na
msimamo mkali, lakini jambo la kuzingatia ni kuwa usikae na mtu ambaye
unaamini hatakutimizia kile ambacho unategemea kukipata mwishoni. Pia
weka uwiano katika kumtafuta mtu ambaye atakufanya wewe kuwa ni mwenye
furaha bila ya kutoa baadhi ya vitu amabvyo ni vya thamani kwako kwake.
4. TAFUTA MTU UNAE
ENDANA NAE KITABIA.
Kuendana
kitabia ni jambo la muhimu sana na ni jambo linaloimarisha sana uhusiano, hivyo
basi unapomtafuta yule wa pekee kwako anatakiwa kuwa ni yule ambaye
mtashirikiana nae katika mambo yako unayoyapenda. Hii itakupa uwezo wa kujua
mambo anayoyapendelea yeye pia na hata katika kupanga mipango kwa pamoja
kwa urahisi zaidi.
5. SHIRIKIANA NA MARAFIKI
Mahusiano
ya kichumba maranyingi yamekuwa yakitokana na marafiki wawili wa jinsi ya
tofauti. Ingawa inaweza kuonekana kuwa si kawaida, unaweza kuishia kumuoa
rafiki wa binamu yako. Hivyo yakupasa kuwa mkweli kwa marafiki zako, ambao
wanakujua kikwelikweli jisi ulivyo na mtu unayetaka kuwa nae. Au waweza kukutana
na moja ya marafiki zako ambaye waweza kumwambia juu ya mtu ambaye umevutiwa
nae, usiwe na aibu au uoga kwa yule anaekufanya wewe kuwa na
furaha duniani nao wakati mwingine wanaweza kuhusika kukusaidia hata namna ya
kumpata unayemtaka badala ya wewe kuhusika sana lakini pia itakuwa ni njia
mojawapo wewe kupata taarifa ambazo kwa namna moja ama nyingine isingekuwa
rahisi kuzipata.
6. AINISHA SIFA AMBAZO HUPENDI UMPENDAYE AWENAZO.
Sifa
ambazo hupendi yule umpendaye awe nazo ni muhimu sana kuwa miongoni mwa sifa
unazozizingatia wakati unapochagua mchumba wa kuwa nae maishani. Unapoanza
kuangaza huku na kule, yule ambaye utamkabidhi moyo wako ni vizuri kuzingatia
vitu ambavyo vitaimarisha uhusiano wenu kuwa imara bila kukatishwa kwa namna
iwayo yote. Na hapa yapo mambo ya kuzingatia-:
a. UKOSEFU WA MVUTO
Mvuto
wa nje unaweza kukua siku hata siku lakini hautathiminiki. Ingawaje mtu
anaweza kukidhi vigezo kadhaa unavyovitaka lakini kumbuka kuwa huwezi
kujilazimisha mwenyewe kuwa na mvuto kwa mtu mwingine.
b. KUKOSA MWAFAKA.
Kukosa
mwafaka juu ya jambo fulani linalowahusu. Mtu asiye kuwa na siri, mtu mwenye
vurugu na asiyekuwa na subira katika mambo fulani fulani na pia
asiyeuzuia mdomo wake katika kuropokaropoka, hilo ni tatizo kubwa,yakupasa kuwa
mwangalifu. Lakini huwezi kujua kwasababu unaweza usikubali vitu fulani fulani,
lakini kama lipo jambo ambalo linakufafanua kuwa wewe ni nani ambalo mwenzi
wako mtarajiwa halitmbui, pia utakuwa na tatizo katika siku zijazo.
c. UTOFAUTI KIMAZINGIRA.
Unaweza
kumpata umpendaye wa maisha yako yote, lakini anaishi sehemu ambayo hata kwa
hali yoyote hutaweza kufika kwa mfano wewe uko Tanzania na yeye yuko Uingereza
huwezi fika kirahisi , haitakusaidia kwa namna yoyote bali utapoteza muda bure.
Katika
kumtafuta yule umpendaye kijana yeyote unayetamani kuwa na mwenzi unayemtaka
unapaswa kuwa mwangalifu sana maana hapa ndipo watu wengi hupoteza dira
kwasababu walichagua chuma cha kutu badala ya dhahabu yaani yule waliyemdhania
kuwa ndiye anafaa kumbe sivyo kamawalivodhani. Hivyo basi hiki kipengele
kinahitaji umakini wa hali ya juu. Hitimisho la mahusiano ya kiuchumba linaweza
kuwa chungu, na hivyo basi kupelekea kutafuta msaada kwa wazazi, washauri na
marafiki kwa usaidizi na hii ni kwasababu ya kukosa umakini katika swala hili
kama kutokufuata njia sahihi wakati wa kumtafuta yule umpendaye. Hivyo
uangalifu mkubwa unatakiwa ili kuzuia kuingia katika shimo hili kubwa lenye
maumivu makali yasiyokuwa na dawa ya kutuliza maumivu hayo. Ni imani yangu
ni kuwa kupitia nja tulizoziona hapo juu zikizingatiwa kwa umakini
na kama zilivyo kwa hakika zitakusaidia kumpata yule umpendaye kwa dhati
popote pale ulipo.