Kumtafuta mwandani wa moyo wako kwenye mtandao ni jambo la kuvutia sana; japokuwa kuna umuhimu wa kupata hatari. Kwasababu tayari una aina nyingi ya watu, lakini pia huna uzoefu wa kukutana na jamii kubwa ya watu na unawakati mgumu kupambanua ni mtu yupi anakidhi vigezo vya mtu unayemtafuta. Sasa yapo mambo ya kuzingatia katika matazamio yako ya kumtafuta mchumba wako ndani ya mtandao. Hivi vitu adimu ambavyo naenda kukupa vitakusaidia kukuweka mbali na mwanaume au mwanamke ambaye siye unaye mtafuta.
Jambo la 1.
Anza taratibu. TAMBUA HII kuwa kuna aina ya yote ya watu katika himaya ya mapenzi; na siyo watu hawa wote watakufaa. Chukua muda wako –kama umekutana na mtu kwa mara ya kwanza na anza mazungumuzo ama kuchati naye taratibu na kumgundua kama ndiye. Mtu huweza kujisifu kuwa yeye yuko hivi ni mpaka wewe umgundue hivyo na sisitiza kuwa chukua muda wako kumchunguza kwa makini tabia yake ya mwazo na ya sasa. KAMA KUNA KITU kimekutatiza ni RAHISI TU achana naye. Chukua virago vyako. KAMWE USIKIMBILIE MAHUSIANO YOYOTE YA KIMAPENZI KABLA YA KUFIKIRIA KWANZA.
Jambo la 2.
Linda Utambulisho wako (protect your Identity). Moja ya faida ya kumatafuta umpendaye kwenye matandao ni kwamba utajikuta unamjua mtu haswa kulingana na haiba yake. Inabaki kuwa uamuzi wako kuwa ni wakati gani kujionyesha kuwa wewe ni nani haswa lakini yakupasa kuwa makini sana, Ingawa pale mtu anapopokea haiba (personality) anaweza kuitumia kinyume na matwakwa yako. Kama mwenzako anakupa presha juu ya wewe kumpa jina lako la mwisho, email yako, anwani ya nyumbani kwako, namba ya simu, na mahala ambapo unafanyia kazi na vitu vinginevinavyokutambulisha wewe…ACHANA NA HUYO MTU.
Jambo la 3.
Tumia Akili. Wakati unapozungumza na mtu kupitia himaya ya Mapenzi, usitupe maamuzi mazuri mbali eti kisa hii ni huduma ya kimtandao. Jambo ambalo linaweza sikika vizuri na likahamasisha ni kuwa umempata mtu ambaye umemjua vizuri. Kuwa na tahadhari na uzitumie hizo tahadhari, na USIANGUKE katika kumpenda mtu eti kwasababu umevutiwa na wasifu wake uliousoma kwenye mtandao. Chukua muda wako pia pitia kila maeneo muhimu.ya chaguo zako. Baada ya kufanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha vya kutosha. Ni mazoea sana watu huanguka katika mapenzi baada ya mazunguzo ya kwanza. USIRUHUSU HILI. Jitahidi kudumisha akili yako na kuona kuwa kumtafuta umpendaye kwenye mtandao ni sawa na utafutaji wa mchumba ndani ya dunia yetu hii ya kawaida. Haipaswi kupenda kila wasifu unaousoma.
Jambo la 4.
Omba Picha. Unapokutana na mtu, chati naye, na ona jinsi mwanzo wa mahusiano unavyokuwa unajengwa hapo itakupeleka kuona kuwa unaweza ukaomba picha. Hii itakupelekea hasa kukupa taarifa zaidi kuhusu mtu mwenyewe kuliko email na chating zingine zinazofanyika. Awali ya yote itaondoa uongo wa kila mtu anavyomtazamia mwenziye kuwa yukoje. Utajua pia anakuvutia kimuonekano? Ama La! Mwisho kama anashindwa kutuma picha yake, huenda kukawa na sababu. NENDA KWA UANGALIFU
Jambo la 5.
Kuwa Makini. Hili linawezekana, ni jambo la muhimu sana ukilifuata. Katika email, kila mtu anaweza kusikika vizuri lakini katika uhalisia si yeye .mnapokuwa umejiingiza katika himaya ya uchumba ama mapenzi na mtu pia tegemea bendera nyekundu ama tabia za zamani. Pia weka umakini katika majaribio yoyote ya kukupa presha ama kukutawala. Mwisho angalia sana na kuwa makini na taarifa zile ambazo mchumba wako anakupatia ama majibu ya maswali unayomuuliza. Kama uhusiano wako unaonyesha mambo yafuatayo. Unashauriwa kuangalia upya mahusiano yako;
1. Kama mwanamke/ mwanaume hatoi majibu ya kweli kuhusu umri wake, vitu anavyopendelea, mwonekano, taaluma yake na ajira yake.
2. Kama anakataa kuongea na wewe kwenye simu baada ya kuanzisha mahusiano ya kwenye mtandao.
3. Kama hatoweza kujibu kwa ufasaha maswali mtakayokuwa mnaulizana. Je atakuwa anakujibu maswali vizuri ama anakurudishia swali kwako.
4. Kama atakupa picha ya kikundi cha watu waliyopiga pamoja na yeye akiwemo itakayofanya kuwa vigumu kumtafuta.
Kutafuta mchumba mzuri umpendaye kwenye mtandao ni jambo zuri na linahamasisha na linatimiza ndoto zako. Wewe kumbuka tu kufuata mambo muhimu hapo juu na fanya kama yanavyoelekeza na utafanikiwa.